Pages

Tuesday, 4 June 2019

Mwanaume hafundishwi kupenda ila mwanamke hufundishwa


kama kichwa cha uzi kisomekavyo kiufupi naweza sema katika mahusiano ni mwanaume ndiye amfundishaye mwanamke kupenda kwa sababu zifuatazo

-Kwa asilimia kubwa katika mahusiano unakuta mwanaume kamtongoza mwanamke ambaye hakuwa na hisia juu ya mwanaume huyo ila mwanaume ndiye aliyekuwa na hisia za kimapenzi utakuta mwanamke anamkubali kwanza huyo mwanaume si kwa kumpenda ila tu kuna sababu mbalimbali kama vile kwa kujaribu tu kupima mwanaume huyo anaupendo kiasi gani sasa pale mwanaume atakapoonesha mapenzi motomoto mwisho unakuta mwanamke naye anakuja kwa kasi kumpenda huyo mwanaume na hapa ndio unakuja kuona a love graph reads inversely propotional kwasababu mwanaume atanza kushuka na mwanamke ataanza kupanda

- Mwanaume anaweza lialia na kubembeleza penzi kwa mwanamke ambaye hana hisia na huyo mwanaume mwishoe akamkubali na kumpenda lakini mwanamke kama hukupendwa na mwanaume umpendae hata ukajilizaje na kujitishia kujiua huyo mwanaume hawezi akampemda huyo mwamamke kamwe

-Mwanamke anaweza lazimishwa kuolewa na mwanaume asiyempenda kwa mwanzo ataona shida sana ila kwa baadae ataanza mpenda mumewe taratibu na mwisho anampenda mazima ila mwanaume mkimlazimisha kuoa mwanamke asiye mpenda atamnyanyasa tu hawezi kumpenda hata akaishi nae miaka mia

Namaliza kwa kusema 99% ya wanawake huolewa na wanaume wasio wapenda ila huwapenda kwa baadae na 99% ya wanaume huoa wanawake wawapendao

JUA NYOTA YAKO YA KIMAPENZI


  Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.
Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.

Tabia Za Watu Na Alama Za Nyota
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:
Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20
Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19
Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20
Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22
Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22
Mashuke(Virgo):Agosti 23 – Sept 22
Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22
Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21
Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan 19
Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18
Makundi Ya Alama Za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:
Moto:Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
Maji:Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
Hewa:Imara na yenye kukuza au kuendeleza
Udongo:Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.
Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto: Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi
Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:
Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”: Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
Yenye Kubadilika “Mutable”: Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
Isiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki
 Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo
Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.
Haiba Na Tabia Za Alama Za Nyota
#1 Nyota Ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19
alama-za-nyota_kondoo
Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
Kiongozi
Muongeaji
Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
Mwaminifu kwa marafiki na familia
Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi
 #2
Nyota Ya Ng’ombe: Aprili 20 -Mei 20
alama-za-nyota_ngombe
Ni alama ya udongo:
Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
Makini na muangalifu
Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
Mstahimilivu
Mwenye kutegemewa
Ni mgumu kubadilika
Anapenda vitu vizuri na vya thamani
Unapenda urembo na vitu vya kupendeza
Mwenye hisia zilizofichika
Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.
 #3 Nyota Ya Mapacha: Mei 21 – Juni 20
alama-za-nyota_mapacha
Ni alama ya hewa:
Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
Anafikiri kwa haraka na mcheshi
Ni mwasilianaji mzuri
Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
Hana utulivu
Ana mipango na malengo makubwa
Mwenye kubadilika kirahisi
#4 Nyota Ya Kaa: Juni 21 – Julai 22
alama-za-nyota_kaa
Ni alama ya maji:
Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amani
Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
Ana huruma
Ni mwangalifu
Mkimya na
 #5  Nyota Ya Simba: Julai 23 – Agosti 22
alama-za-nyota_simba
Ni alama ya moto:
Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.
Anapenda kuonekana na watu
Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
Mwenye matumaini mazuri
Mwenye kuheshimika
Mshindani
Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
Mwenye mvuto
#6 Nyota Ya Mashuke: Agosti 23 – Septemba 22
alama-za-nyota_mashuke
Ni nyota yenye alama ya udongo
Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
Wanajali afya
#7 Nyota Ya Mizani: Septemba 23 – Oktoba 22
alama-za-nyota_mizani
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.
Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.
Husimamia haki na usawa
Anapenda sanaa na urembo
Wabunifu wa sanaa
Ni mpenzi wa muziki
Ni muwazi katika kuonyesha upendo
Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
Mpenda amani
Wenye mvuto wa kupendwa
#8 Nyota Ya Ng’e: Oktoba 23 – Novemba 21
alama-za-nyota_nge
Ni alama ya nyota ya maji na ni mwenye hisia nzito
Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
Anapenda malumbano makali
Wanatumia nguvu
Jasiri
Wastahimilivu
Washindani
Wanauwezo ,
Wachunguzi wa mambo
Wasiri
Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
Wanajitegemea
Ni wenye maamuzi
#9 Nyota Ya Mshale: Novemba 22 – Desemba 21
alama-za-nyota_mshale
Ni alama ya moto na ni mwenye mapenzi mazito na vitu
Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
Ni mwenye kupenda uhuru
Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
Rafiki
Mwenye ari
Hawana utulivu
Waaminifu na wakweli
Wanapenda safari
#10 Nyota Ya Mbuzi: Desemba 22 – Januari 19
alama-za-nyota_mbuzi
Ni alama ya udongo na mwenye kuhitaji nyumba yenye amani ili kuhisi ukamilifu.
Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
Mgumu kubadilika
Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
Mfanyabiashara
Mwajibikaji
#11 Nyota Ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18
alama-za-nyota_ndoo
Ni alama ya hewa:
Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
Wakipekee
Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
Mwenye huruma
Muona mbali
Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
Ana utu na mwenye kudai haki
Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
Anapenda sanaa na maisha ya anasa.
#12 Nyota Ya Samaki: Februari 19 – Machi 20
alama-za-nyota_samaki
Ni alama ya maji na ni mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo.
Ni mkweli na mwenye hisia nzito
Hana ubinafsi
Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
Mpenda amani
Ana huruma
Anajitoa
Wana ndoto
Wabunifu
Wana aibu

Maswali 40 Ya Kumuuliza Mwanamke Mnapokua Out

Ushawahi kutoka deti na mwanamke halafu ukafikia mahali katika chat yenu unaishiwa na maneno ya kuongea?

Ama umeagana na mwanamke mtoke deti siku ya pili halafu umekuwa ukikesha siku nzima ukiwaza ni maneno ama ni usemi gani utakaoongea siku ya pili wakati ambapo mtakutana?




Well, usiogope. Hapa umefika kwa zahanati ambayo itakutibu matatizo yako.

Hapa tumekuandalia maswali 40 ambayo utayatumia kumuuliza mwanamke na kuyafanya maongezi yenu yavutie na kumfanya mwanamke apendezeke na wewe hadi mwisho.

Well. Kabla ya kuorodhesha maswali haya kuna mambo ambayo unapaswa kufahamu:


Anza kwa kumsifia ama kumpendezea kwa mambo anayofanya mfano unaweza kumsifia vile alivyovalia, kazi yake, umbo lake nk.
Wakati utakapokuwa unamuuliza mwanamke haya maswali, hakikisha ya kuwa unatoa nafasi ya angalau sekunde 30 kabla ya kumuuliza swali la pili, yaani usimmiminie maswali yote wakati mmoja.
Hakikisha kuwa haulazimishi maswali yako, mwanamke akikataa kujibu swali lako jipe shughli kiasi kv unaweza kucheza na vidole vyako ama jambo jingine kabla kumuuliza swali lingine.
Baadhi ya mambo ambayo pia unapaswa kuzingatia katika rodha ya maswali haya ni kuwa:

Unapaswa kuyachanganya maswali yako. Maswali tuliyoyaorodesha hapa ni maswali yaliyowazi, yaani yanaweza kupanuliwa yakazua mada nyingine. Anza na maswali sahili kuangalia iwapo mwanamke unayezungumza naye anapenda kuongea au la. Pia muulize maswali yaliyo wazi ili kuongeza hoja yako.

Usimakinike na orodha ya haya maswali. Tumia maswali machache ambayo unayaona unaweza kuyatumia halafu ujeuza mada yako uanze kuongea maswala yako. Ukimakinika kutaka kutumia maswali haya yote basi unaweza kumfanya akuone hauvutii na anaweza kuboeka na wewe haraka sana.

Usihifadhi maswali haya. Hili ndilo jambo baya zaidi la kufanya. Ukikaa na deti wako huku ukirudia swali la kwanza hadi jingine unaweza kumfanya mwanamke aone kwamba unamfanyia mahojiano ya kazi. Unachohitajika ni kusoma baadhi ya maswali haya, yahifadhi kwa simu yako halafu yatumie wakati ambapo maongezi yako yanafifia.


Maswali yenyewe ni kama ya fuatayo...

1. Unaipenda hii sehemu?

2. Huwa unapenda kunywa kinywaji gani?

3. Mapochopocho unayoyapenda ni yapi?

4. Ushawahi kuja hii sehemu awali?

5. Siku yako ilikuwaje?

6. Unafanya kazi wapi?

7. Huwa unapenda nyimbo aina gani?

8. Unapenda salad aina gani?

9. Ni mkahawa gani unaoupenda zaidi?

10. Ni movie aina gani unapenda kuangalia zaidi?

11. Ni mambo gani unapenda kufanya baada ya kutoka kazini?

12. Unafanya mambo gani ili kujifurahisha?

13. Ulisomea wapi?

14. Sehemu gani unaipenda sana zaidi kwa likizo zako?

15. Ni kitu gani unapendekezea ili kuinjoy siku yako?

16. Je wewe ni mtu wa kufuga mnyama gani? Paka ama mbwa?

17. Kama ungetawala dunia, ungetaka kubadilisha kitu gani?

18. Mapenzi mazuri ni yapi kulingana na mtizamo wako?

19. Mzazi gani yuko karibu na wewe?

20. Ni kitu gani kinachokuboa kwa mwanaume?

21. Unapenda kuvalia kikazi ama kimtaa?

22. Unawachukuliaje wanawake ambao wanapenda maringo?

23. Hivi ni kweli kuwa wewe unakuwa mrembo hivi?

24. Je wewe ni mtu wa kusoma ama wapenda kucheza games?

25. Ni mtu gani katika maisha yako ambaye unampenda zaidi?

26. Unapenda mambo ya ghafla ghalfa ama mpangilio?

27. Ni nani huwa unaongea naye kama unapata changamoto katika mapenzi?

28. Je una kumbukumbu yeyote ya utotoni mwako ambayo inakufanya utabasamu unapoifikiria?

29. Ukisafiri katika hii dunia, ungetamani usikose nchi ngapi tano?

30. Ni kitu gani kinakufurahisha maishani mwako?

31. Je, wewe uko karibu na familia yako?

32. Ni kitu gani unachochukia zaidi kuona wakati unapokutana na deti wako mara ya kwanza?

33. Je wewe ni mtu wa kurauka mapema ama kuchelewa usiku zaidi?

Haya yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kumuuliza deti wako iwapo ameingiliana na mazungumzo yako. Maswali haya yanaweza kuwa ya ucheshi, mengine yanaweza kuchangia kuongeza mazungumzo na baadhi yanaweza kubashiri vile ambavyo deti yako itakuwa mbeleni na huyu mwanamke.

34. Ni sehemu gani ya mwili wako huwa inatekerenyeka zaidi ikiguswa?

35. Ulikuwa miaka mingapi mara ya kwanza ulipohisi kupenda mtu flani?

36. Ni kitu gani kinachofanyika kawaida unapokuwa na marafiki zako wa kike mkiwa mnapokula bata?

 37. Kimtizamo wako, maana ya mahusiano ni nini?

38. Hivi, mahusiano yako ya awali yalichukua muda gani?

39. Deti yetu ya leo umeiona vipi kabla tumeet tena wakati mwingine?

40. Sahizi unafikiria nini?

ZIJUE SABABU 7 ZA USALITI KATIKA MAPENZI (NDOA) ILI TUPUUNGUZE USALITI

Tatizo la usaliti limekuwa ni kubwa sana katika mapenzi. wengi wamekuwa wakilalamika kuhisi kusalitiwa na wapenzi wao.zamani wanaume ndio walikuwa wakiongiza katika usaliti kwa wake zao ,lakini utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa  nao wanawake wamekuwa wasaliti katika ndoa zao Na hii ndio sababu iliyonifanya niandike sababu za usaliti katika mapenzi

Kutoridhika katika tendo la ndoa.

 Ni dhahiri kuwa mmoja wapo asipotosheka kila mnapokutana ,nakama hiyo hali itaendelea bila ufumbuzi basi yule asiyeshiba katika hayo mapenzi atatafuta njia ya mkato(michepuko)
Kutopata mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda.-Wengine hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.
* TABIA YA UCHAFU WA MWILIU, kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke-


*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa

*Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri (masomo
Kuna watu wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya kwa wanandoa.

*Tamaa ya mali na vitu vya thamani(utajiri wa haraka):
 Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia wanaume wenye magari, wenye fedha ..
*Kujifunza mambo au mitindo mipya
-Wakati mwingine kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.
*Kutopata tendo la ndoa muda mrefu,
 labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k-Hata hivyo kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi wake afurahie

SMS ZA KUMTOA NYOKA PANGONI

nakupenda, niamini mpenzi
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*

upendo ni jibu kwamba kila mmoja anataka. . . .
upendo ni lugha ,
kwamba kila mmoja anaongea,
upendo hauwez kununuliwa,
na isiyo kadirika na ya bure,upendo kama uchawi safi,ni
siri ya maisha matamu
nakupenda mpenzi
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
"Mimi sitaki kuwa kila kitu kwa kila mtu, lakini napenda
kuwa kitu kwa mtu.na mtu mwenyewe ni wewe"
nakupenda laazizi
"Kama mimi nilikuwa na maua kila wakati
mawazo yangu
yangekuwa juu yako,nisingefikiri wa kumpa mwingine kabla
yako je wewe ungekuwepo nayo
ungempa nani kwanza? "
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
ningependa nikuambie neno ambalo halina gharama na
likutumiwa vibaya halina maana wala thamani. neno hilo
haliandikiki kwenye karatasi wala hata halitamkiki ila tu
Linatokea Bila kujua na halina sababu.neno hilo mi
mwenyewe silijui ila ndo linatufanya tuwe pamoja Japo tupo
Kasi Na Kusi. Nakupenda sana Dear Figganigga
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua
nafsi nikupende wewe pekee,nafunga milango ya moyo wangu
ili
kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako
mpenzi.nakupenda sana laazizi
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
sipo tayari kuukabidhi moyo wangu kwa mwingine zaidi
yako,wewe ni wa pekee maishani mwangu mwenye kujua hisia
moyoni mwangu
mpenzi nipende daima pendo lako nitalienzi, nakupenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini
yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si
njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa
unaempenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi ni safari=unifanye nauli ya moyo, mapenzi ni
maradhi=unifanye daktari ni kutibu maradhi yako,mapenzi ni
kiu=niwe maji jangwani,mapenzi ni chakula=nikulishe
maishani mwako na uwe asali moyoni mwangu
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
wengi hupenda fanta kwa ladha yake,wengine hupenda
pilipili kwa muwasho wake,wengine hupenda asali kwa utamu
wake ila mimi nakupenda wewe kwa upendo wako.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
nimetuma ndege wangu auzunguke ''moyo'' wako kwa '' upendo
'' auguse ''uso'' wako kwa ''faraja'' na mwisho
akunong'oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi ni utoto,deka ulie nitakubembeleza,mapenzi ni
zawadi tabasamu nibusu niambie kiasi gani unanpenda,naweza
kusema asilimia kubwa jina lako limezunguka kuta wa moyo
wangu.kamwe jina lako haliwezi kufutika.nakupenda sana Figganigga
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
teke la kuku halimuumzi mwanaye sawa na dhati ya mapenzi
haiumzi moyo wa ampendaye,tugombane sasa hivi tupatane
badaye,najua hakuna wasiogombana ,kama wapo siku
wakigombana wataachana.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
yapitayo mdomon yametokea moyon,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Furaha yangu ni kuwa nawe kwani u zaid ya mboni
yangu,najisifu kuwa nawe maishani mwangu naamini itatokea
kutokuwa mbali nawe mpz wangu,unisahaulishe machungu na
karaha za huu ulimwengu .nakupenda dia

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

>>--------->>> Mshale huu unamtafuta mtu muhimu sana ktk
maisha yangu na kama umekutana nao
usiukwepe uache
uchome Moyo wako gharama
za matibabu juu yangu.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

sioni zawadi ya kukupatia kwa mapenzi
unayonipatia,
moyoni nimekuridhia wewe pekee penzi langu daima
kukupatia nakupenda
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
hakika kama ni mume MUNGU kanipatia,kuwa nawe najiona
kama malkia ,nakupenda mpz na daima nitaenzi penzi
lako.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Nina habari nzuri nataka kukuambia kuna mgeni leo kaja
kunitembelea,nguo nyekundu amevalia yaani!utamu wako kwa
sasa siwezi kukupatia
kwa maana mgeni kashakuharibia
nakupenda dear

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Ni yangu mazoea kila cku cm yako
kuipokea kama si meseji
kunitumia
leo naumia kila napo fikiria nini
kimetokea hadi
mawasiliano yetu
yameanza kupotea,sawa tu.naamini hali
ya kawida itarejea
na
majonzi moyoni yatanipotea
nakupenda mpz
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Nimezunguka pande zote za Tanzania macho
nikiyaangaza
kumsaka mrembo
wakumkabidhi wangu moyo wenye upendo
ndani yake na kulila
TUNDA lake
kwa nafasi huku nikimpa mahaba ya dhati na sikuwahi kuhisi
kama wewe ndiye
ulie uteka moyo wangu.
nakupenda laaziz
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Raha ya ucngz ni ucngz . . . .''tamu''ya penzi ni ndoto .
Na furaha ya ndoto ni yule umpendaye kwa dhati,nitafurahi
nikiwa mimi,
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Kipepeo kipeperushe kunipenda maamuz yako kamwe usijute
nakupenda mpz moyoni mwako unitulize.
Nakupenda mpz
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Moyo wangu unajua kupenda katu haujui kutenda
mpz,nakupenda tukwepe fitina mpz.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Nenda sms taratibu kwa yule ma BEST nimpendaye,ukimkuta
amelala ucmuamshe mpige busu kisha mnong'oneze mwambie
nampenda sanaaaa
Nilivyokutana nawe cku ya kwanza nilikupenda kwa dhati
,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni mwako,cwezi
kuchezea nafac hyo laaziz nitakushika daima.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Je unakubali au unakataa kwa mujibu wa sheria ya mahakama
ya mapenzi kifungu cha mahaba unahukumiwa kuwa na mimi
milele,unaweza kukata rufaa kama hujatendewa haki.sawa?
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbal
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi wangu!
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
kamwe cwez kuacha kukupenda,utaendelea kujificha moyo
mwangu cku zote za maisha yang,maana wewe ndiye mhimili wa
maisha yangu,tafadhal naomba unipende milele!
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
mapenzi ni upepo,mimi sivumi na kupotea,mapenzi ni mahaba
sili nikamaliza,mapenzi ni raha kamwe cwez
kuipeza,nakupenda wewe pekee

UKIMTUMIA MPENZI WAKO SMS HIZI , LAZIMA AJE AKUPE ZAWADI YA SITA KWA SITA

SMS nzuri ya kumuuliza mpenzi wako kama anakupenda kweli kwa moyo wake wote

Mapenzi mazuri yanasifa zifuatazo, kuridhishana, kupeana
bila kubaniana, kubusiana, kuheshimiana, kujaliana, kusubiriana, kusikilizana. je utaweza kunifanyia yote hayo? nijibu mpenzi.



Meseji ya kumsisitiza mpenzi wako muendelee kupendana


wengi walisema penzi letu lisingedumu,lakini leo twawaacha
midomo wazi kwa misengenyo yao isiyo na maana ,tuendelee
kupendana,wanafiki roho ziwaume!


SMS ya mapenzi ya mahaba kwa mpenzi wako aliyeko mbali


Kuna bahari kati yetu. Misitu na milima inatutenganisha,
mimi si ‘Supamani’ lakini nipe sekunde moja nitavuka nchi
nyingi kukutumia mapenzi yangu. Umeipata hiyo? Pokea mapenzi yangu japo uko mbali.


Meseji ya kumwambia mpenzi wako kuwa hutamuacha


Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu peke yako dear…


SMS nzuri ya kumtumia mpenzi wako ya kumuomba aje kwako


Mpenzi usiende mbali nami,njoo ufaidi utamu usioisha
hamu,nitakupa mwili wangu ucheze nao hadi
asubuhi,nitakulisha unachokitaka,sitakubania kwani naogopa
wengine wanaweza kukupa… .njoo leo uniambie unataka
nini?


SMS nzuri ya kumwambia mpenzi wako jisni anavyokuchanganya kwa unavyompenda


Watu waliniambia ninaweza kufanya chochote kama tu
nitaweka mawazo yangu juu ya hicho kitu. Lakini kila
nikijitahidi unaipoteza akili yangu


SMS ya kumwambia mpenzi wako asijute kukupenda kwani unampenda


Kipepeo kipeperushe kunipenda maamuz yako kamwe usijute
nakupenda mpz moyoni mwako unitulize.
Nakupenda mpz


SMS ya kumtumia mpenzi wako kunapokuwa na wanafiki wanaoingilia penzi lenu


Wanafiki tusiwaombee kifo daima na milele washuhudie penzi
letu linavyozidi kukua,na tunavyopambana na mapito

Mbinu 15 za kumtongoza mwanamke akakupenda daima

Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.

Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.

2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.

3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.

4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.

5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.

6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.

7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.

8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.

9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.

10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.

Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke kama uko na pesa [MTONYO WA KUTOSHA]